Wahesabiwa ambao bado wapewa mwongozo

Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda amesema asilimia 93.45 ya kaya zote Tanzania zimehesabiwa hadi kufikia leo Jumatatu Agosti 29, 2022 saa 2 asubuhi. Makinda amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya Sensa ya Watu na Makazi.Sensa ya Watu na Makazi ilianza Jumanne ya Agosti 23, 2022 na itahitimishwa leo“Zoezi la kuhesabu watu lililoanza usiku wa kuamkia tarehe 23 Agosti 2022 hadi kufikia 29 Agosti, 2022 linaendelea vizuri ambapo kiwango cha kaya ambazo zimehesabiwa kimefikia asilimia 93.45.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda amesema asilimia 93.45 ya kaya zote Tanzania zimehesabiwa hadi kufikia leo Jumatatu Agosti 29, 2022 saa 2 asubuhi.

 Makinda amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya Sensa ya Watu na Makazi.Sensa ya Watu na Makazi ilianza Jumanne ya Agosti 23, 2022 na itahitimishwa leo

“Zoezi la kuhesabu watu lililoanza usiku wa kuamkia tarehe 23 Agosti 2022 hadi kufikia 29 Agosti, 2022 linaendelea vizuri ambapo kiwango cha kaya ambazo zimehesabiwa kimefikia asilimia 93.45.

Amesema taarifa zilizokwishakusanywa zinaonyesha bado kuna asilimia 6.55 ya kaya ambazo hazijahesabiwa.

“Inawezekana tusiweze kufikia kaya zote zilizobaki kwa leo na lengo letu ni kuhakikisha kila mtu anahesabiwa.”

Ametoa wito kwa wananchi ambao hawajahesabiwa kutoa ushirikiano kwa makarani waliopo katika maeneo yao ili wahesabiwe kabla ya leo jioni.

Kuhusu ambao hawatahesabiwa

Makinda ametoa muongozo kwa wananchi ambao watakuwa hawajahesabiwa mpaka kufikia leo jioni kuwa bado wana nafasi ya kuhesabiwa akitoa utaratibu ikiwamo kwenda kwenye ofisi za serikali za mitaa wanakoishi

“Mwananchi unashauriwa uende moja kwa moja kwenye Ofisi za Serikali za mitaa onana na Mwenyekiti au Mtendaji wa Mtaa unaoishi na hakikisha unawachia namba ya mawasiliano ili karani akufuate ulipo na kuanza kazi ya kukuhesabu”

“Kwa maeneo ya vijijini mwananchi ambaye hajahesabiwa aende kwenye ofisi ya mwenyekiti wa kitongoji anachoishi acha namba ya mawasiliano ili makarani wakufuate ulipo ili wakuhesabu”. 

Pia, Kamisaa huyo amesema wananchi wanaweza kupiga simu kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kutoa taarifa kuwa hawajahesabiwa.

Sensa ya Majengo kuanza kesho

 Makinda amesema sensa ya majengo nchini itaanza kesho Jumanne Agosti 30, 2022 na itafanyika kwa siku tatu

Kama mnavyofahamu Serikali imepanga pia kufanya Sensa ya Majengo mara tu baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu. Sensa hii itajumuisha kukusanya taarifa za majengo yote ya makazi na yasiyo ya makazi nchi nzima kwa ajili ya kuboresha Sera na kupanga mipango ya kimkakati ya kuboresha sekta ya nyumba nchini.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii