WIVU WA MAPENZI, USHIRIKINA VYATAJWA KUWA NDIO CHANZO CHA MAUAJI.

Wakati kumekuwa na wimbi la mauaji nchini, Serikali imesema sababu za wananchi kujichukulia hatua mkononi ni wivu wa mapenzi, migogoro ya ardhi, ulevi na imani za kishirikini.
Kauli hiyo imefuatilia, swali lilioulizwa leo Jumatano Septemba 14, 2022 na Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso ambaye ametaka kufahamu nini kauli ya Serikali katika kutatua changamoto ya wimbi kubwa la mauaji hapa nchini.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Hamad Hassan Chande, amesema ni kweli kumekuwa na ongezeko la matukio ya mauaji hapa nchini.
“Matukio mengi yanasababishwa na wananchi kujichukulia sheria mkononi, wivu wa mapenzi, migogoro ya ardhi, ulevi na imani za kishirikina,”amesema.
Baada ya majibu hayo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema licha ya Serikali kuchukua hatua bado linaendelea kukuwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii