Papa aelekea Kazakhstan kushiriki mkutano wa kimataifa wa dini

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameanza leo ziara ya siku tatu nchini Kazakhstan ili kushiriki mkutano wa kimataifa wa kidini. Hata hivyo Papa Francis hatakutana na kiongozi wa Kanisa la Orthodox la Urusi kama ambavyo ilitarajiwa awali. Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki aliondoka Rome na ujumbe wake mapema leo. Baada ya kutua katika mji mkuu wa Kazakhstan Nur-Sultan, atakutana na Rais Kassym-Jomart Tokayev na wanadiplomasia. Kwa papa huyo mwenye umri wa miaka 85 ambaye ana matatizo ya goti na anatumia muda mwingi akiwa kwenye kiti cha walemavu, itakuwa ni ziara yake ya tatu ya kigeni katika mwaka wa 2022, kufuatia ziara ziara zake za Malta na Canada. Mkutano wa Viongozi wa Ulimwengu na Dini za Jadi unatarajiwa kufanyika katika mji huo wa Nur-Sultan.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii