Mwanasarakasi wa Kike Asiye na Miguu Aliyeweka Rekodi Duniani

 Jen Bricker au Moceanu ni  mhamasishaji na mwanasarakasi wa kike kutoka Marekani asiye na miguu yote miwili.

Jen ana umri wa miaka 32, ni mwanamke aliyepitia mateso na manyanyaso tangu utotoni mwake, kwani alipozaliwa wazazi wake walimtelekeza kutokana na ulemavu wake.Alilelewa na wazazi baki, ambao ni Sharon na Gerald. Wawili hao walimlea na kuhakikisha anatimiza ndoto zake kama watoto wengine.

Jen, alipata matumaini ya kuishi na kupambania ndoto zake, alijiunga na michezo ya mazoezi ya viungo pamoja na sarakasi.


Alipofikisha umri wa miaka 10, alishiriki mashindano ya kimataifa ya michezo ya sarakasi. Alifanikiwa kushinda na kuwa binadamu wa kwanza asiye na miguu kushinda taji hilo duniani kote.


Umaarufu wake ulimfanya akutane na marafiki pamoja na mume wa maisha yake kutoka Australia.

Baada ya miaka kadhaa, alikutana na mama yake mzazi halisi, wakati baba yake mzazi akiwa ameshafariki dunia.

Mama alimueleza Jen kuwa walimtelekeza ili kukwepa gharama za matibabu kutokana na ulemavu wake.Jen, aliamua kuandika kitabu cha “Everything is posible” ili kuhamasisha watu kutimiza ndoto zao bila kujali changamoto za kimaumbile walizonazo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii