KISINDA AKWAMA YANGA

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imekata mzizi wa fitina kwa kuuzuia usajili wa winga aliyerejea Yanga, Tuisila Kisinda na kupeleka usajili huo hadi dirisha dogo.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho ni kwamba Yanga imekwama kumtumia Kisinda katika kipindi hiki na sasa itasubiri hadi dirisha dogo ili iweze kumtumia mchezaji huyo baada ya kukamilisha majina 12 ya wachezaji wa kigeni kama sheria inavyotaka.

Yanga iliipeleka pingamizi la Kisinda kutaka atumike kutokana na kuwahi dirisha kubwa la usajili kabla halijafungwa Agosti 31 ikimsajili kwa mkopo kutoka RS Berkane ya Morocco, lakini imekuwa tofauti kutokana na jina la mchezaji huyo kushindwa kupenya kwenye usajili kutokana na klabu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii