Rais wa Marekani Joe Biden amempongeza William Ruto kwa kuibuka mshindi wa uchaguzi wa urais.
Katibu katika White House Karine Jean-Pierre alisema Marekani inasubiri kuendeleza urafiki wake na Kenya.
alisema urafiki wa Kenya umejengwa kwenye msingi wa demokrasia na utekelezaji wa kisheria na wanatarajia hilo litaendelea.
Ikulu ya Marekani pia imemshukuru kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga kwa kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Upeo.
Biden anasema yuko tayari kuendelea kufanya kazi na Ruto baada ya kuunda serikali yake akipaishwa Septemba 13.
"Marekani na Kenya zina uhusiano wa miaka mingi unaotokan na kutetea demokrasia, usalama na kukuza uchumi. Tunasubiri kuendeleza uhusiano huu na Rais Ruto na serikali yake mpya," alisema Biden.
Ruto alitangazwa mshindi wa urais Agosti 15 baada ya kupata kura milioni 7.1 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga wa Azimio la Umoja aliyepata 6.9M.