Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amefahamisha kupitia barua iliyoonekana na shirika la habari la Reuters,kwamba nchi yake itasadia katika juhudi za kuyatathmini upya madeni ya Sri-Lanka na kuihakikishia kuipatia fedha nchi hiyo ya kisiwa inayokabiliwa na mgogoro. Yellen amesema,Marekani ambayo ni mkopeshaji iko tayari kushiriki kwenye mpango huo wa kuisadia Sri Lanka katika suala la madeni yake na kuzitolea mwito nchi nyingine wakopeshaji kutoa ushirikiano kikamilifu katika mazungumzo na kulitazama upya deni la nchi hiyo. Sri Lanka inapambana kujitowa katika mgogoro mbaya wa kiuchumi ambao haujawahi kuonekana kwa miongo saba. Wiki iliyopita nchi hiyo ilifikia makubaliano ya awali na shirika la fedha la kimataifa IMF ya kupata mkopo wa kiasi dola bilioni 2.9