Gavana wa Kenya afukuza maafisa wakuu kwa kuchelewa mkutanoni.

Gavana mteule wa Kenya amejizolea sifa kwa sheria kali za afisini baada ya kuwafukuza maafisa wakuu kwa kufika kwenye mkutano dakika chache baada na yeye kuingia.

Gavana George Natembeya wa kaunti ya Trans-Nzoia, magharibi mwa Kenya, aliamuru milango ifungwe kwa yeyote anayefika baada ya saa 09:00 saa za eneo hilo, muda uliowekwa wa mkutano huo.

Mkutano huo na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kaunti, sawa na mawaziri, ulikusudiwa kujadili mpango wa maendeleo wa kaunti kwa miaka mitano ijayo.

“Ninaposema tukutane saa tatu kamili asubuhi namaanisha saa tatu asubuhi wala sio na dakika moja juu. Binafsi nilifika hapa dakika tano kabla ili kila mtu ajifunze kutunza wakati. Baada ya wakati uliowekwa, ikiwa uko nje, baki huko,” Bw Natembeya alinukuliwa akisema na wahudumu wa eneo hilo.

Gavana huyo alipata sifa kwa ukali wake katika jukumu lake la awali kama msimamizi wa serikali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii