Mahakama ya katiba nchini Angola imetupilia mbali madai ya chama cha upinzani UNITA kuyafuta matokeo ya uchaguzi yaliyokipa ushindi chama tawala cha MPLA. UNITA ilipeleka malalamiko yake mahakamani baada ya tume ya uchaguzi wiki iliyopita kumtangaza rais Joao Lourenco kushinda muhula wa pili madarakani, ikitoa hija kwamba tume hiyo haiku-kishirikisha ipasavyo katika hatua za mwisho za kuidhinisha matokeo. Hata hivyo mahakama ya katiba Angola imesema chama cha UNITA kinachoongozwa na Adalberto Costa Junior hakikukidhi matakwa yaliyohitajika ili kuwezesha matokeo hayo kufutwa. Matokeo ya tume ya uchaguzi yaliyotangazwa wiki iliyopita yalikipa ushindi chama cha MPLA kwa asilimia 51.17 ya kura na UNITA ikapata asilimia 43.9 ya kura.