Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameahidi kufanya kazi na Rais Mteule William Ruto pamoja na Naibu Rais mteule Rigathi Gachagua, baada ya Rais Uhuru Kenyatta kustaafu hivi karibuni.
Kwenye taarifa alioandika katika mtadao wake wa kijamii, siku ya Jumatatu, Septemba 5, Museveni alimpongeza Ruto baada ya Mahakama ya Upeo kuafiki ushindi wake wa kuingia Ikulu.
"Nilimpigia simu Mheshimiwa William Ruto kumpongeza kwa uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Upeo ya kuafiki ushindi wake wa kuwa rais wa tano wa Kenya," Museveni alisema.
Museveni aliahidi kufanya kazi na Ruto kwa minajili ya kuboresha mikakakti ya ushirikiano wa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Museveni, ambaye amekuwa Rais tangu mwaka wa 1986, ni mmoja wa marais Afrika Mashariki amnaye amehudumu kwa kipindi kirefu.
Museveni amefanya kazi na marais watatu wa Kenya, akianza na Daniel Moi, Mwai Kibaki na Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta.