Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula ameagiza kuondolewa kazini Mkurugenzi wa Tehama wa wizara hiyo, Venance Mwolo kwa kile alichifafanua kuwa hatoshi katika majukumu hayo.
Mabula ameyatoa maelekezo hayo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Allan Kijazi leo Jumanne Septemba 6, 2022 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
"Mkurugenzi wa Tehama simtaki katika wizara ya ardhi, ameshindwa kutekeleza majukumu yake. Katibu Mkuu (Dk Allan Kijazi), wasiliana na utumishi wafanye utaratibu wa kuleta mtu mwingine," amesema.
Ametaka Mkurugenzi atakeyeletwa kuifanya kazi hiyo ahakikishe anaendana na kasi ya Serikali katika matumizi ya Tehama.