CHAMA CHA NCCR- MAGEUZI KUITISHA KIKAO WIKI IJAYOM, MBATIA ANAHUSIKA.

Kwa miezi kadhaa sasa, chama cha NCCR- Mageuzi kimekumbwa na mgogoro uliokigawa makundi mawili, moja linaloungwa mkono na Mwenyekiti Mbatia, la pili ni lile linaloungwa mkono na Katibu Mkuu wake, Martha Chiomba.

Kundi hilo la Martha linalomhusisha pia Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini ndilo linaloonekana kuwa na nguvu kubwa na baraka za Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini Tanzania.

Hii inathibitishwa na ukweli kuwa kikao cha Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi cha Mei 21, mwaka huu kilichomsimamisha uongozi Mbatia na Makamu Mwenyekiti wake Tanzania Bara, Angelina Mtahiwa, kilihudhuriwa na Naibu Msajili, Sisty Nyahoza na alikitambua.

Wakati NCCR-Mageuzi upande unaoungwa mkono na ofisi ya Msajili ukiitisha mkutano mkuu utakaofanyika jijini Dodoma wiki ijayo, kumekuwa na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Mbatia anajiandaa kujiunga na Chadema.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii