Watakaosalimisha Silaha Wanazomiliki Kinyume cha Sheria Kusamehewa.

Jeshi la Polisi linapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa kutakuwa na uzinduzi wa kampeni maalum ya mwezi mmoja unaojulikana kama msamaha wa Afrika itakayohusisha usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari zinazomilikiwa na baadhi ya watu kinyume cha sheria, ama kwa kutokujua taratibu za kisheria za umiliki wa silaha.

 

Akitoa taarifa hiyo jana Septemba 03 mwaka 2022 msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP, David Misime amesema uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika kesho Septemba 5 kuanzia saa tatu asubuhi katika Viwanja vya Mashujaa mkoa Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (MB).

 

Aidha Misime amesema baada ya uzinduzi huo tushirikiane sote kuelimishana kuwa yeyote atakayesalimisha silaha anayomiliki kinyume cha sheria katika muda utakaotolewa na Mhe.Waziri siku hiyo, hatochukuliwa hatua yeyote ile.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii