Serikali ya Tanzania imesema asilimia 50 ya mahitaji ya mbolea ya ruzuku imeshaingizwa nchini kabla ya msimu wa kilimo wa 2022/23 kuanza.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa Serikali kutoa ruzuku katika mbolea ili kuwapunguzia wakulima bei zilizopanda kutokana na majanga ya kidunia ambapo Sh150 bilioni zilitengwa kufanikisha hilo.
Septemba 2, 2022, Tanzania ilipokea tani 31,000 ya mbolea ya kupandia aina ya DAP kutoka kampuni hiyo, katika Bandari ya Dar es Salaam kupitia meli ya MV Clipper Clyde.
Katika mazungumzo yake wakati wa upakuaji wa mbolea hiyo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema tayari tani 150,000 ya mbolea hizo ipo katika maghala mbalimbali nchini kwa ajili ya kuuzwa kwa wakulima.
Alisema Tanzania inahitaji kati ya tani 400,000 hadi 500,000 za mbolea ili kukidhi haja ya wakulima wote, kabla ya msimu kuanza tayari asilimia 50 ya mbolea hiyo imeshaingia nchini.