Qatar yaruhusu Bia wakati wa Kombe la Dunia.

Qatar itawaruhusu mashabiki kununua bia zenye kileo katika mechi za soka za kombe la dunia saa tatu kabla ya kuanza na kumalizika kwa filimbi ya mwisho, lakini sio wakati wa mechi.

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limesema hapo jana kwamba mashabiki wataruhusiwa kununua bia katika maeneo maalumu yaliyotengwa katika viwanja lakini sio ndani.

Michuano ya kombe la dunia mwaka huu inafanyika kwa mara ya kwanza katika nchi ya Kiislamu yenye udhibiti mkali wa unywaji pombe, na hivyo kutoa changamoto kwa waandaji wa hafla inayofadhiliwa na kampuni kubwa ya bia.

Katika mashindano mengine yaliyopita, bia zilikuwa zikiruhusiwa kuuzwa ndani ya viwanja muda wote.

Qatar imefanya kampeni ya miaka 12 ili kuwa mwenyeji wa kwanza wa kombe la dunia katika eneo la Mashariki ya Kati.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii