Raila Odinga Kuhutubia Taifa Leo Adhuhuri Baada ya Rais Kutangazwa.

Kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja one Kenya Raila Odinga ametangaza kuhutubia taifa leo, Jumanne, Agosti 16.

Mgombea huyo wa mara tano wa urais atahutubia taifa saa chache baada ya mgombea urais wa Kenya Kwanza William Ruto kumshinda katika uchaguzi wa taifa.


Kiongozi huyo wa ODM, kupitia mkurugenzi wake wa mawasiliano, alisema atazungumza kutoka Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta saa mbili usiku leo, Jumanne.

"Hotuba ya Kiongozi wa Muungano wa Azimio La Umoja Rt Raila Odinga kwa Taifa. Saa: 2pm," ujumbe wa Onsarigo ulisema.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii