Ujumbe wa Wabunge watano wa Marekani umekutana leo na Rais wa Taiwan Tsai Ing-Wen mjini Taipei na kuzua hasira ya China, ikiwa ni wiki mbili tu baada ya ziara ya Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi. Wizara ya ulinzi ya China imesema ziara hiyo inafichua sura ya Marekani kama mzua vurugu na mhujumu wa amani katika rasi ya Taiwan. Beijing imefahamisha leo kuwa itaanzisha tena luteka za kijeshi kufuatia ziara ya wabunge hao wa Marekani. China inakichukulia kisiwa hicho kama himaya yake na imeapa siku moja kukitwaa, lakini Taiwan inajitambua kama taifa huru na la kidemokrasia.