Umoja wa Ulaya umesema mamlaka ya Taliban "imekiuka na kudhulumu kwa kiwango kikubwa haki za wanawake na wasichana wa Afghanistan." Hayo yamo katika taarifa ya msemaji wa umoja huo kwa masuala ya kimataifa, Nabila Massrali, ikiwa kabla ya maadhimisho ya kwanza ya mwaka mmoja tangu mamlaka hiyo iingie madarakani.Taarifa hiyo imeongeza kwa kusema Wataliban wameshindwa kuanzisha mfumo shirikishi wa kisiasa, jambo ambalo linakwenda kinyume na matarajio ya raia wa Afghanistan.Kesho Jumatatu, Afghanistan itakuwa inaadhimisha mwaka mmoja tangu kundi la Taliban lichukue hatamu ya uongozi, mwezi Agosti mwaka uliopita, huku kukielezwa haki za msingi za wanawake zikikandamizwa, uhuru wa vyombo vha habari ukibinywa na sehemu kubwa ya taifa hilo ikitumbukia katika lindi la umasikini.