Vyombo vya habari nchini Iran vimeripoti kwamba, Iran imemfungulia mashtaka mwanasiasa mwanamageuzi Mostafa Tajzadeh, ambaye aliwahi kufungwa na pia kukamatwa tena mwezi uliopita akituhumiwa kuhujumu usalama wa taifa.Duru zinaeleza Tajzadeh mwenye umri wa maka 65 ambaye mwaka jana aliingia katika mchakato wa kuwania urais bila mafanikio kama mwanamageuzi na mfungwa wa kisiasa kwa miaka saba alifikishwa mahakamani mjini Tehran jana Jumamosi.Mwanasiasa huyo aliwahi kuwa naibu waziri wa mambo ya ndani katika kipindi cha miaka ya 1997-2005 wakati wa utawala wa rais mwanamageuzi, Mohammad Khatami.Alitiwa mbaroni mwaka 2009 wakati wa maandamano ya kupinga kuchaguliwa tena kwa rais wa wakati huo Mahmud Ahmadinejad, ambayo yalipingwa na upinzani unaounga mkono wagombea wanamaeguzi ambao hawakufanikiwa, Mehdi Karoubi na Mir Hossein Mousavi.