Venezuela na Colombia zipo katika jitihada ya kurejesha mahusiano

Mataifa ya Venezulea na Colombia kila moja, limeteuwa balozi wake kuyawakilisha katika miji mikuu ya mataifa hayo kwa kujenga upya uhusiano baina ya mataifa hayo mawili, ambao ulivunjika miaka mitatu iliyopita.Uteuzi huo unafanyika siku chache baada ya kuapishwa kwa Rais wa kwanza wa mrengo wa kushoto wa Colombia, Gustavo Petro, ambaye alionesha nia yake ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Venezuela.Serikali ya Venezuela ilivunja uhusiano wake na Colombia mapema 2019 baada ya wapinzani wa Venezuela kujaribu kuvuka mpaka wa Colombia, wakiwa na malori yenye shehena ya vyakula.Serikali ya Maduro ilisema msaada huo ulifutikiza jaribio la mapinduzi ambalo lilikuwa linaungwa mkono na serikali ya Marekani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii