Klabu ya Simba imeomba Radhi kwa Waumini wa Dini ya Kikristo Sakata la Msalaba


Klabu ya Simba imeomba radhi kwa Waumini wa Dini ya Kikristo, Viongozi wa Madhehebu yote ya Kikristo, Serikali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania na Jamii kwa ujumla kwa usumbufu uliojitokeza kwenye Tamasha la Simba Day August 08 mwaka huu.

Katika Tamasha hilo Msanii Tunda Man aliingia Uwanjani kutumbuiza akitumia mavazi na vifaa na ishara ambayo imeibua hisia za kuwakera wengi hasa Waumini na Viongozi wa Dini ya Kikristo.

“Kwa kuheshimu imani za Watu wote tumelazimiia kuomba radhi kwa tukio hilo, hata hivyo Simba hatukufahamu kama Tundaman atatumia aina hiyo ya maudhui kwani siku ya majaribio hakufanya hivyo”

“Vilevile tumewataka Wasanii hao waombe radhi kwa Hamii ambapo wamekiri na kuahidi kufuata hatua stahiki katika kuomba radhi na kujutia kosa hilo”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii