Pelosi kuzuru Japan baada ya Taiwan

Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi amesema leo mjini Tokyo kuwa Marekani "haitairuhusu" China kuitenga Taiwan, baada ya ziara yake katika kisiwa hicho kinachojitawala kuikasirisha China.Pelosi ameongeza kuwa China inaweza kujaribu kuizuia Taiwan kutembelea au kushiriki katika maeneo mengine, lakini hawataitenga kwa kuzuia ziara nchini humo. Spika huyo amesema kuwa walikuwa na ziara za ngazi ya juu, maseneta wakati wa msimu wa masika, na ziara za kuendelea na kwamba hawatairuhusu China kuitenga Taiwan.Hapo jana, Pelosi alikutana na viongozi wa kisiasa wa Korea Kusini mjini Seoul. Pelosi pia alikutana na spika wa bunge la kitaifa la Korea Kusini Kim Jin-pyo pamoja na wabunge wengine wakuu. Kim amesema Pelosi pia alielezea wasiwasi kuhusu kuongezaka kwa vitisho vya nyuklia kutoka Korea Kaskazini. Hata hivyo hakuzungumzia kuhusu ziara yake Taiwan. Pelosi pia alitembelea eneo lisilo la kijeshi kwenye mpaka na Korea Kaskazini. Kwasasa kuna wanajeshi 28,500 wa Marekani nchini Korea Kusini, mshirika muhimu wa Marekani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii