mchezaji wa mpira wa kikapu Brittney Griner ahukumiwa miaka 9 jela

Hukumu ya mchezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani Brittney Griner kwenda jela miaka 9 nchini Urusi kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya, katika muktadha wa mahusiano yenye mvutano mkubwa na Urusi, imesababisha watu wengi kutoa hisia zao nchini Marekani.


Ikulu ya White House ilikuwa ya kwanza kujibu kwa taarifa kwa vyombo vya habari. Hukumu hiyo sio ya kushangaza kwa Joe Biden. Hukumu ya kwenda jela ni ukumbusho wa yale ambayo kila mtu tayari alijua: Urusi inamshikilia Brittney Griner inyume cha sheria.

Rais wa Marekani anatoa wito wa kuachiliwa mara moja ili aweze kuungana na mkewe, familia, marafiki na wachezaji wenzake. Lawama kama hizo zimetolewa naWaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye anaelezea wasiwasi wake kuhusu mfumo wa mahakama ya Urusi na utaratibu wake wa kuumia nguvu. Kamati ya masuala ya mambo ya nje ya Bunge la Seneti imetumia neno "mateka" kuhusu kesi ya Brittney Griner, bingwa wa Olimpiki mara mbili na ulimwengu umeitaka Urusi kumuuachilia huru mara moja bila masharti. .

Maafisa wa Marekani wanakumbusha kwamba pendekezo la kubadilishana wafungwa liko mezani: Brittney Griner na Mmarekani mwingine, Paul Whelan, ambaye yeye mwenyewe anatuhumiwa kwa ujasusi, dhidi ya mfanyabiashara wa silaha Viktor Bout, alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela nchini Marekani. Urusi kwa sasa yenye uamuzi. Kwa maneno mengine, uamuzi unategemea kutoka moja kwa moja kwa Vladimir Putin.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii