Zaidi ya vijana wadogo 2,000 waliondoka nchini mwao na kuelekea Italy.

Zaidi ya vijana wadogo 2,000 wa Tunisia walivuka bahari ya Mediterania mwaka huu kutoka katika taifa lao la kaskazini mwa Afrika kuelekea Italy kutafuta maisha bora, shirika la kutetea haki za binadamu limesema Jumatano.

Jukwaa la Tunisia la haki za kiuchumi na kijamii (FTDES) limesema watoto wadogo ni miongoni mwa jumla ya wahamiaji 10,139 wa Tunisia ambao walipita kwenye bahari ya Mediterania kuelekea Italy tangu mwanzoni mwa mwaka 2022.

Zaidi ya wahamiaji 14,700, wakiwemo wengi kutoka mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, walizuiliwa na kurejeshwa nyuma katika kipindi hicho, FTDES imesema.

Umaskini unaochochewa na mzozo mbaya wa kiuchumi na kijamii unafanya hatari za bahari kuwa sababu ya pili kwa wahamiaji hao ambao wana ndoto ya maisha bora kwao wenyewe na watoto wao,” FTDES imesema.

Imekemea pia “siasa zisizo za kibinadamu za Umoja wa Ulaya, ambazo zinazuia uhuru wa kutembea wa wahamiaji.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii