Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Real Madrid, Samuel Eto'o amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT).
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon amewahi kushinda tuzo ya mchezaji Bora Afrika mara nne mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010.