Serikali ya Misri imesema Rais wa taifa hilo, Abdel Fattah al-Sisi leo hii anakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa mataifa matano ya Kiarabu, mkutano ambao unatarajiwa kuiangazia vita ya Ukraine na athari zake kwa nishati na shida ya upatikanaji chakula.Taarifa hiyo imewataja watakohudhuria mkutano huo wa pwani ya kaskazini/mashariki mwa Cairo, kuwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mohamed bin Zayed Al-Nahyan, Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhemi, Mfalme wa Jordan, Abdullah II na kadhalika Mfalme Hamadi wa Bahrain. Taarifa ya ofisi ya rais wa Misri, imesema jana Jumatatu viongozi hao tayari wamekutana rais wa Misri na kufanya mazungumzo mafupi yenye shabaha ya kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina ya mataifa yao.