Waandamanaji dhidi ya gharama kubwa ya maisha wataka Waziri Mkuu ajiuzulu

Waandamanaji dhidi ya gharama kubwa ya maisha wamevamia mitaa mbalimbali ya miji ya Port-au-Prince, Les Cayes, Cap-Haitien na Gonaïves. Raia wengi walijitokeza barabarani siku ya Jumatatu, kushutumu gharama ya juu ya maisha, kupanda kihalisi kwa dola ya Marekani dhidi ya gourde (fedha za Haiti), na kutaka Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry aondoke madarakani mara moja.

Shughuli zote za biashara zilisitishwa. Katika mji wa Gonaïves, kulionekana mawingu ya moshi mweusi, vizuizi vilivyochomwa moto, vikiwekwa kila kona ya barabara. Wakiwa njiani, waandamanaji waliendelea kuimba "ikiwa bei za mahitaji ya kimsingi hazitashuka, shule wanafunzi hawata kwenda shuleni mwezi Septemba". 

"Leo tuko mitaani kutuma ujumbe kwa mamlaka," alisema mmoja wa waandamanaji. Kesho, bado tutakuwa mitaani. Maduka yote lazima yakatize shughuli zao. Tunadai kujiuzulu kwa Ariel Henry. Baada ya kuwa madarakani kwa zaidi ya mwaka mmoja, hawezi kutusaidia chochote. Alisema anaweza kufanya uchaguzi, bado hakujafanyika uchaguzi. Na ikiwa hakuna uchaguzi, nchi haitaendelea popote. »

"Sote tutakufa njaa"

“Unapokuwa na gourde 1,000 (fedha za Haiti) mfukoni mwako, huwezi kununua chochote. Sote tutakufa njaa. Huwezi tena kununua kipande cha sabuni ya kufulia kwa gurde 60, kipande  kimoja cha sabuni kinauzwa gourde 80. Watoto wangu hutembea mitaani na nguo chafu. Hakuna kazi nchini. Tunatakiwa kuwasha moto kila mahali ili kumfukuza Ariel Henry madarakani, "amesema.

Waandamanaji wameipa serikali hadi hadi Ijumaa, Agosti 26 kujibu madai yao, bila hivyo wametishia kuharibu maduka.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii