IGP Wambura apewa maagizo haya na Makamu wa Rais Dkt. Mpango

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, amemuagiza IGP Camillius Wambura, kuangazia malalamiko yote yanayotolewa na wananchi kwa jeshi la polisi na kuwachukulia hatua askari wachache wanaoharibu taswira ya jeshi hilo.

Kwa mujibu wa Eatv. Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 18, 2022, alipokutana na kufanya mazungumzo na na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillius Wambura, na kulitaka jeshi la polisi kutenda haki pasipo kuonea mtu yeyote na yeyote anayevunja sheria achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na sio vinginevyo.

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amelipongeza jeshi la polisi kwa kuendelea kuimarisha amani pamoja na ulinzi wa wananchi na mali zao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii