Kanali Mtanzania Atunukiwa Medani na Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani

Wizara ya Ulinzi ya Jeshi la Shirikisho Urusi limemtunuku nishani kwa kuimarisha ushirikiano katika Majeshi Kimataifa.

 

Kanali Joseph Bakari ni mwanajeshi anayetumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania anayefanya kazi nchini Urusi.

Kanali Bakari ambaye ni Mkurugenzi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) alitunukiwa Nishani hiyo kutokana na mchango wake na juhudi zake katika kusimamia maandalizi ya Michezo ikiwemo ya Maofisa wanafunzi yaliyoafanyika Nishani hiyo alivishwa na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la Shirikisho la Urusi Jenerali Nikolay Pankov mbele ya viongozi mbalimbali wa Jeshi la Shirikisho la Urusi pamoja na wageni wengine wakiwemo washiriki kutoka nchi 20.

 

Aidha, nishani hiyo pia hutunukiwa wananchi wa Shirikisho la Urusi na mashirikisho ya Kimataifa na raia wa nchi nyingine ambao wamechangia kutekeleza kwa mafanikio jukumu maalum la Jeshi la Shirikisho la Urusi Kimataifa. urusi hivi karibuni.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii