Elon Musk kuhusu kuinunua Manchester United, hapana nilikuwa natania

Bilionea namba moja duniani mwenye utajiri wa $265.7 bilioni Elon Musk amekanusha kuhusu kuinunua klabu ya Manchester United baada ya kuandika kupitia akaunti yake ya Twitter. Mwanzilishi wa Tesla alitoa maoni hayo katika tweet ya usiku wa manane.

Musk aliandika: “Ili kuwa wazi,ninaunga mkono nusu ya kushoto ya Chama cha Republican na nusu ya kulia ya Chama cha Kidemokrasia! “Pia, ninainunua Manchester United karibu nawe.

Ujumbe wake, ambao ulizua gumzo mitandaoni, ulivutia watu wengi kwa kasi na kupokea retweets zaidi ya 36,000 na karibu likes 200,000 ndani ya saa chache.

Baadae baada ya kuandamwa na meseji za mashabiki wa United walimuuliza ni kweli anataka kuinunua Manchester United? alijibu “hapa ni mfululizo utani tu wa hapa Twitter, siwezi kununua klabu yoyote ya mpira”

Klabu hiyo  ya ligi kuu ya uingereza iliyokuwa ikimilikiwa na familia ya Glazer yenye maskani yake Florida tangu 2005.

Umiliki wao umekuwa ukishutumiwa mara kwa mara na mashabiki kutokana na deni, mgao na usimamizi mbaya uliofuatia ununuzi wao uliozua utata.

Glazers pia wamesimamia kushuka kwa kasi kwa maonyesho na matokeo katika miaka ya hivi karibuni.

Rekodi ya mabingwa hao mara 20 wa Uingereza hawajashinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza tangu msimu wa mwisho wa Sir Alex Ferguson mwaka 2012-13 na hakuna aina ya fedha kwa miaka mitano.

Mashabiki wa Manchester United waliendelea kumshawishi mtandaoni baada ya kumueleza namna gani klabu hiyo ilivyotajiri wa mashabiki wengi hivyo endapo angeinunua basi angepata faida mara dufu

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii