Man United Yaachana na Rabiot Kisa Mshahara Mkubwa, Yamfungia kazi Casemiro

Baada ya mazungumzo kwa siku kadhaa na klabu ya Juventus pamoja na muwakilishi wa mchezaji Adrien Rabiot ambaye ni mama yake, Klabu ya Manchester United imeshindwa kufikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo licha ya kufikia makubaliano ya mauzo ya mchezaji huyo na klabu yake ya Juventus.

 

Imeelezwa mazungumzo kati ya Man United na mchezaji huyo yamekwama kutokana na kiasi kikubwa cha malupulupu anachokihitaji ili ajiunge na wakali hao wa Manchester jambo ambalo limewafanya Manchester United kusitasita kwenye kukamilisha dili la uhamisho wa mchezaji huyo.

 

Inaripotiwa klabu hiyo yenye makazi yake jijini Manchester imepanga kuongeza mchezaji mkongwe mwenye uzoefu katika eneo lao la kiungo kabla dirisha la usajili halijafungwa, kwa sasa inasemekana klabu hiyo imeelekeza nguvu zake kwa kiungo Mbrazil anayecheza katika klabu ya Real Madrid Carlos Henrique Casemiro.

Adrien Rabiot


Kulingana na madhaifu makubwa kuonekana katika safu ya kiungo ya timu hiyo Manchester United wamedhamiria kwa dhati kufanya usajili msimu huu, ndiyo sababu iliyopelekea kuhusishwa na wachezaji wengine kadhaa akiwemo Frenkie De Jong na Moises Caicedo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii