MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amewasili mkoani
Katavi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi itakayokwenda sambambamba na
kupokea taarifa na kukagua miradi ya maendeleo.
Katika ziara hiyo
ya kikazi ameongazana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho
Shaka Hamdu Shaka na baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege Katavi
Kinana amepokelewa na Wana CCM Mkoa wa Katavi wakiongozwa na Mwenyekiti
wa Chama Mkoa Beda Katani.
Baada ya kuwasili Kinana akiwa na
Shaka wamepata nafasi ya kusailiamana na wanachama wa Chama hicho na
kisha kupokea taarifa ya CCM na Serikali Mkoa wa Katavi.
Akipokea
taarifa hiyo Kinana ameelezwa hali ya mwenendo wa Chama na Serikali na
kwa sehemu kubwa ameambiwa hali ni shwari na kwamba viongozi wamekuwa na
ushirikiano mkubwa hali inayofanywa utekelezaji wa Ilani kufanyika kwa
kiwango cha kuridhisha.
Kwa mujibu wa ratiba Kinana ambaye
ameanza ziara leo Julai 25 ,2022 akiwa mkoani hapa mbali ya kupokea
taarifa ya Chama na Serikali atazindua mradi wa fremu 15 za biashara,
pia atatembelea mradi wa fremu za vibanda 188.
Aidha Kinana
atazindua kituo cha afya na kuzungumza na wananchi na wanachama, pia
baadae atazungumza na WanaCCM na viongozi mbalimbali . Kinana atakuwa
katika ziara ya mikoa ya Nyanda za Juu ukiwemo Mkoa wa Katavi na kisha
kuelekea Mkoa Rukwa, Songwe na Mbeya.