Korea Kaskazini yaishtumu Marekani kwa kutengeza silaha za kibaiolojia Ukraine

Korea Kaskazini leo imeishutumu Marekani kwa kutengeneza silaha za kibaiolojia nchini Ukraine na kurejelea madai ya Urusi yaliyopuuziliwa mbali na Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Machi. Shirika la habari la nchi hiyo, KCNA, limeripoti kuwa Marekani imejenga maabara nyingi za kibaiolojia katika nchi na maeneo kadhaa, ikiwemo Ukraine, na hivyo kukiuka mikataba ya kimataifa. Mnamo mwezi Machi, Urusi iliishutumu Marekani kwa kufadhili utafiti wa utengenezaji wa silaha za kibaiolojia nchini Ukraine, madai iliyoyatowa mwezi mmoja baada ya uvamizi wa Urusi kwenye taifa hilo.Marekani na Ukraine zimekanusha uwepo wa maabara hizo za kutengenezea silaha za kibaiolojia, huku Marekani ikisema madai hayo yanaonesha kuwa huenda Urusi ikatumia mbinu hiyo. Mnamo mwezi Machi, Izumi Nakamitsu, afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kukomesha mashindano ya silaha alisema kuwa Umoja huo haufahamu kuhusu mpango wowote wa silaha za kibaiolojia nchini Ukraine..

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii