Mahakama ya Uturuki yaafiki uamuzi wa Erdogan kufuta mkataba wa kuwalinda wanawake

Mahakama ya juu ya Uturuki imeunga mkono uamuzi wa rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan wa kuiondoa Uturuki katika mkataba wa Ulaya dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia. Uamuzi huo wa Erdogan alioufanya mwaka jana ulilaaniwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na serikali za magharibi. Hata wapinzani wa rais huyo walitilia shaka ikiwa anayo mamlaka ya kuiondoa nchi katika mkataba wa kimataifa kwa kutumia agizo la rais. Lakini mahakama ya juu ya Uturuki imetupilia mbali rufaa dhidi ya uamuzi wa Erdogan, iliyojumuisha ushahidi kutoka kwa wasomi na mashirika maarufu ya wanawake, kwa hoja kuwa uchunguzi wa kisheria hauwezi kuutengua uamuzi wa rais. Wakili wa vuguvugu la kupinga Uturuki kujiondoa katika mkataba huo wa Ulaya amesema uamuzi wa mahakama ya juu umeipuuza katiba ya nchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii