Yemen zaongoza muda wa kusitisha mapigano kwa miezi mingine miwili

Umoja wa Mataifa umesema pande hasimu kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen zimekubaliana kuongeza muda wa mkataba wao wa amani kwa miezi mingine miwili. Awali, serikali inayofadhiliwa na Saudi Arabia na waasi wa Kihouthi wanaofadhiliwa na Iran walisaini makubaliano ya kusitisha mapigano mapema mwezi Aprili. Mkataba huo wa mwezi mmoja ndio uliokuwa muda mrefu kabisa wa amani ndani ya kipindi cha miaka saba ya mapigano. Uamuzi wa kuongeza muda wa mkataba huo hapo jana, ulifikiwa masaa machache kabla wa awali kumalizika muda wake. Mkataba mpya wa sasa utaendelea hadi tarehe 2 Oktoba. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen amesema mazungumzo ya kina kuelekea kuongezwa muda wa mkataba huo lilikuwa sehemu ya masharti ya makubaliano yenyewe. Pande zote mbili, serikali na Wahouthi, zinalaumiana kwa kutoheshimu kikamilifu makubaliano ya mkataba huo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii