Pelosi awasili Taiwan licha ya onyo la China

Licha ya vitisho kutoka Beijing, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, amewasili kwenye kisiwa cha Taiwan. China ilionya kuwa ingelichukuwa hatua kali endapo Pelosi angeliitembelea Taiwan. Beijing inakichukulia kisiwa hicho chenye serikali yake ya ndani kuwa sehemu ya mamlaka yake. Muda mchache kabla ya kuwasili kwa Pelosi, shirika la habari la China liliripoti kwamba ndege za kijeshi za nchi hizo zilikuwa zimevuuka Lango Bahari la Taiwan, ambao unazitenganisha pande hizo mbili. Pelosi ni afisa wa juu kabisa wa Marekani kuitembelea Taiwan ndani ya kipindi cha robo karne. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 alisema lengo la ziara yake ni kuunga mkono demokrasia ya Taiwan. Mivutano kati ya China na Taiwan na hivyo pia na Marekani, imekuwa ikiongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii