Wasiolipia Chakula Shuleni Kufungwa Jela.

Halmashauri ya manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro , imepitisha rasimu ya sheria ndogo inayotaka wazazi watakaoshindwa kuwalipia vyakula watoto wao wakiwa shuleni, wafungwe miaka miwili gerezani.

Hayo yamesemwa na kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Sifael Kulanga  ambapo ameeleza kuwa rasimu hiyo inaandaliwa mchakato kupitishwa rasmi na Waziri mwenye dhamana ili iwe sheria kamilili .

 Katika rasmu hiyo, inaonesha mzazi anaweza kutozwa faini isiyopungua shilingi 200,000 na isiyozidi 1,000,000 au kifungo kisichopungua mwaka mmoja na kisichozidi miaka miwili au adhabu zote mbili kwa pamoja.

Kulanga amesema ,rasimu  hiyo imelenga kuhakikisha wanafunzi awali hadi sekondari wanapata chakula shuleni kama moja ya jitihada za kuongeza viwango vya taaluma shuleni.

"Katika rasimu hii wazazi watalipa kiasi cha shilingi 70,000 kwa mwaka ikiw ni shilingi 35,000 kwa muhura kwa wanafunzi wa awali, shilingi 90,000 kwa mwaka kwa elimu ya msingi na shilingi 120,000 kwa sekondari kwa mwaka" Amesema .

Aidha ameeleza kuwa fedha za chakula shuleni zitzsimamiwa na wazazi wenyewe kupitia kamati watakazounda lakini kamati hizo zinaweza kuvunjwa na mkurugenzi wa manispaa iwapo zitaenda kinyume na malengo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii