Bei za mahitaji ya kila siku nchini Ujerumani zinatarajiwa kupungua katika nusu ya pili ya mwaka baada ya mfumuko wa bei wa miezi kadhaa. Taarifa hiyo imetolewa na taasisi ya Ujerumani inayoshughulikia masuala ya kiuchumi.Taasisi hiyo imesema kasi ya mfumuko wa bei nchini Ujerumani imeanza kupungua na inatarajiwa kushuka katika nusu ya pili ya mwaka. Hata hivyo unafuu hautaonekana haraka katika bei za mahitaji ya kila siku kwa muda wa miezi kadhaa. Mfumuko wa bei nchini Ujerumani ulifikia kiwango cha asilimia 7.6 mnamo mwezi huu wa Julai.