Uchumi wa Marekani umenywea tena katika robo ya pili ya mwaka, ishara ambayo katika nchi nyingi duniani inazingatiwa kuwa mdororo wa uchumi. Hata hivyo kusinyaa huko kwa kiwango cha asilimia 0.9 katika kipindi cha miezi mitatu hadi mwezi wa Julai kumesababisha wasiwasi juu ya uchumi wa nchi hiyo. Bei za mahitaji ya kila siku ikiwa pamoja na za chakula na mafuta ya petroli zinapanda haraka kwa kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu mwaka 1981. Licha ya benki kuu ya Marekani kupandisha viwango vya riba ili kuzuia kupanda gharama za maisha bado pana hofu huenda nchi hiyo imeshaingia katika mdodoro wa uchumi hali inayotokea katika nchi ikiwa uchumi haustawi kwa muda wa robo mbili za mwaka mfululizo. Hata hivyo rais Joe Biden amesema uchumi wa nchi yake unaendelea kuwa imara.