Biden, na Xi Jingping wakubaliana kuandaa mkutanao wa ana kwa ana

Rais wa Marekani, Joe Biden na mwenzake wa China, Xi Jingping, wamekubaliana kuandaa mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana, wakati huu Beijing ikiionya Washington kutocheza na kile ilichosema ni “MOTO” kuhusu eneo la Taiwan.Viongozi hawa wamezungumza kwa simu usiku wa kuamkia leo.


Hii ilikuwa ni mara ya tano kwa viongozi hawa kuzungumza kwa njia ya simu au video tangu rais Joe Biden aingie madarakani mwaka mmoja na nusu uliopita, huku ikiwa watakutana itakuwa ni mara ya Kwanza kwao.

Kwa mujibu wa tarifa za maofisa wa Marekani, rais Biden na Xi Jingping, walijadiliana umuhimu wa kukutana ana kwa ana na kuwaagiza wajumbe wa nchi hizo mbili kutafuta wakati muafaka kwa wao kukutana.

Katika mazungumzo yao, rais wa China alirudia tena onyo lake kwa Marekani kuhusu kujaribu kuingilia masuala ya eneo la Taiwan, Jingping akisema nchi yake haitavumilia uchochezi wa aina yoyote.

Kauli kama hiyo pia ilitolewa na rais Biden aliyeionya China kutumia mabavu kuchukua êneo la Taiwan.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii