Ukraine yaanza tena uuzaji wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi

Ukraine imeanza tena operesheni za uuzaji nafaka katika miji kadhaa muhimu ya pwani. Bandari za Odesa, Chernomorsk na Piv-dennyi zinatarajiwa kuanza tena usafirishaji wa nafaka kupitia bahari nyeusi. Hatua hiyo inafuatia makubaliano yaliyofikiwa baina ya Ukraine, Urusi, Uturuki na Umoja wa Mataifa ya kuruhusu mauzo ya nje ya nafaka. Kulingana na Ukraine, meli zilizobeba nafaka zitaanza safari kwa makundi kwa ajili ya usalama. Uturuki nayo imesema kwamba imefungua kituo cha uratibu wa pamoja kulingana na makubaliano. Urusi iliishambulia bandari ya Odesa saa chache baada kusainiwa makubaliano na kuzidisha wasiwasi juu ya utekelezaji wake. Wakati huohuo Rais Volodomyr Zelenskyy ametangaza kuwa Ukraine itaongeza mauzo ya umeme kwa nchi za Umoja wa Ulaya wakati Urusi ikipunguza usambazaji wa gesi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii