Waziri wa Maji Mh. Jumaa H. Aweso (Mb) akielekea Buhigwe kwenye ziara
ya ukaguzi wa Miradi ya Maji amesimama jimbo la Kigoma Kaskazini na
kuzungumza na wananchi wa Vijiji vya Kiganza na Bitale.
Wananchi hao wamewasilisha kero ya kutokuwa na Maji yakutosha katika
maeneo yao kutokana Mkandarasi Serengeti Company Limited kushindwa
kukamilisha ukarabati wa Mradi wa Maji Mkongoro I kwa wakati.
Mradi wa Mkongoro I unatekelezwa na Taasisi ya Enabel kutoka nchini
Ubelgiji na unajengwa na Mkandarasi Serengeti Ltd na kusimamiwa na
Mhandisi Mshauri Howard & Humphrey Consulting Ltd kwa gharama ya
shilingi bilion 2.8
Aidha, Baada ya kuwasikiliza viongozi wakiongozwa na Mhe Mbunge Asa
Makanika, Mh. Waziri ameagiza ndani ya masaa 24 MKandarasi kufika Kigoma
na kukutana na RUWASA pamoja na Enabel ofisi ya Mkuu wa Wilaya chini ya
usimamizi DC kupitia mkataba kwa kina na kuona kama kuna mapungufu
yeyote na kumpatia taarifa ili afanye maamuzi yenye maslahi mapana kwa
wananchi.
Waziri Aweso amewaahidi wananchi kuwa ikibainika kuwa kuna tatizo wahusika wote watachukuliwa hatua mara moja.
Mwisho Waziri amewaahidi wananchi kuwa Serikali inasimamia mradi huo na atahakikisha unakamilika haraka iwezekanavyo.