Zoran avunja ukimya Simba

KOCHA mpya wa Simba, Zoran Manojlovic Maki amevunja ukimya  huku akifichua jinsi alivyouchungulia mziki wa timu hiyo mapema na usajili unaoendelea kikosini akiamini msimu ujao mataji yote yaliyotowekwa Msimbazi yatarejea.

Zoran amepewa mkataba wa mwaka mmoja Simba akichukua nafasi ya Pablo Franco aliyetimuliwa, huku timu ikiwa imepoteza mataji matatu iliyokuwa nayo ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na ASFC.

Mataji hayo yote yamebebwa na Yanga, lakini kocha Zoran akizungumza kwa mara ya kwanza na Mwanaspoti juzi kwa njia ya simu kutoka Serbia, alisema anaamini mataji hayo yatarudi wakijipanga vyema.

Kocha huyo Mreno mwenye asili ya Serbia, alisema ataungana na kikosi hicho Julai 15 katika kambi itakayowekwa Misri kwa maandalizi ya msimu ujao, kwa vile eneo alililopo (Serbia) na Misri ni karibuni kuliko kama angekuja Tanzania kisha kusafiri tena na timu hiyo kambini.

Zoran alisema amekubaliana na uongozi atatambulishwa kwa wachezaji wapya na waliomaliza msimu pamoja wasaidizi wake wa benchi la ufundi wakiwa kambini kisha aanze kazi ya maandalizi ya timu.

“Tutaanza maandalizi taratibu ili wachezaji wazoee mazingira na kupata nafasi ya kujuana ila kadri siku zitakavyoenda tutaongeza kasi kufanya mengi na magumu yakiwa sehemu kubwa ya maandalizi kabla ya kucheza mechi za kirafiki,” alisema Zoran na kuongeza;

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii