Ni mwendo wa tambo na vijembe kuelekea Derby ya Kariakoo.

Ikiwa ni Siku tatu za tambo na vijembe kuelekea kwenye mchezo wa Kariakoo Derby, Simba na Yanga Disemba 11, 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Maofisa habari wa vilabu hivyo wametambiana kuondoka na alama tatu muhimu.

Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ally Shatry amesema, Simba haifungwi mara mbili na Yanga .kwa upande wa Yanga  Hassani Bumbuli amesema kwa maandalizi  waliyofanya basi wataondoka na alama tatu na kushangilia kama mshambuliaji wao Fiston Mayele.

Ally Shatry maarufu kama  ‘Chico’ amesema: "Tunajua Yanga ilitufunga katika mchezo wa Ngao ya Jamii lakini siku zote Simba haifungwi mara mbili. Jumamosi ni zamu yetu maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri. Timu imeingia kambini jana baada ya kurudi kutoka Zambia na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri”.

lakini pia ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema: "Staili yetu ya kushangilia ni ile ile maarufu nchini ya Fiston Mayele, kitu kizuri kinaigwa hata watani mkitaka sio mbaya kuiga. Maandalizi yamekamilika tutamkosa Yacouba Sogne pekee ambaye ni majeruhi wengine wote wapo fiti tayari kwa mchezo. Kwa maandalizi tuliyofanya tunaamini tutaibuka na ushindi”.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 11:00 Jioni Disemba 11, 2021 Jumamosi kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii