OKWA ATUA SIMBA NA MBWEMBWE ZOTE

Mchezaji mpya wa Simba, Mnigeria Nelson Okwa wikiendi iliyopita aliiaga timu aliyokuwa akiichezea ya Rivers United kibabe kwa kuiongoza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, kisha mapema anaanza mchakato wa safari ya kwenda kuanza maisha mapya ndani ya kambi ya Simba iliyopo Ismailia, Misri.

Okwa ni mmoja ya nyota wapya waliosajiliwa na Simba kwenye dirisha hili la usajili litakalofungwa Agosti 31 na mara baada ya mechi ya mwisho na Rivers iliyoitoa Yanga kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, aliwaaga wenzake na benchi la ufundi na fasta jana alichukua usafiri wa ndege kutoka Mji wa Port Harcourt alipokuwa na timu yake ya Rivers kisha akatua Abuja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kusafiri kwenda kambi ya Misri.

Taarifa kutoka Nigeria, zinasema Okwa alibidi afike kwanza Abuja kutokana na kuhakikisha anapata visa ya kuingia Misri ilipo kambi ya timu yake mpya ya Simba ambayo kwa mujibu wa Kocha Zoran Maki itakuwa ya wiki tatu na itacheza mechi zisizopungua tano kabla ya kurejea nchini Agosti 5.

Inaelezwa muda wowote kuanzia sasa kama Okwa atapata visa atatumiwa tiketi ya ndege na mabosi wake wapya wa Simba kisha atatua Misri kwa ajili ya kutambulishwa kama mchezaji mpya wa timu hiyo.

Baada ya zoezi hilo la kutambulishwa kukamilika atajiunga moja kwa moja kwenye mazoezi na wachezaji wenzake kama ambavyo ilivyo

Okwa  alikiri yupo Nigeria kwa ajili ya mambo yake mengine na kama atakuwa mchezaji mpya wa Simba msimu ujao basi hilo si jukumu lake kuweka wazi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii