Ujerumani yaiadhibu Uhispania na hivyo kutinga kwenye robo fainali

Katika mashindano ya kandanda barani Ulaya kuwania ubingwa wa wanawake yanayoendelea huko England jana ilikuwa zamu ya kundi B kucheza mechi zake na kilele cha uhondo wa soka kilikuwa pambano kati ya Uhispania na Ujerumani kwenye uwanja wa mji wa Brentford, wahispania hawakufua dafu mbele ya Ujerumani. Katika dakika ya tatu ya mchuano huo mlinda lango wa Uhispania alifanya kosa pale alipotaka kutoa pasi kwa beki wake lakini mpira ulienda moja kwa moja kwenye miguu ya fowadi wa Ujerumani karibu na lango la Uhispania na akautinga mpira wavuni. Maafa kwa wahispania yaliendelea katika dakika ya 36 ambapo wajerumani walijipatia goli la pili la kichwa. Ushindi huo maana yake Ujerumani itaingia katika robo fainali ambapo itakutana na Finland hapo Jumamosi. Leo jioni Uswisi itapambana na Sweden na waholanzi watakutana na timu ya akina dada wa Ureno.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii