Waziri Mkuu wa Slovania atetea uamuzi wa kufanya matengenezo ya bomba la gesi

Waziri Mkuu wa Slovania, Robert Golob ametetea uamuzi wa kufanya matengenezo ya bomba la gesi linaloleta nishati hiyo kutoka Urusi hadi Ujerumani na ameyapinga madai yaliyotolewa na Ukraine. Waziri mkuu huyo aliyefanya ziara nchini Ujerumani amesema ugavi wa gesi utauimarisha Umoja wa Ulaya na hivyo kuweza kuendelea kuiunga mkono Ukraine. Amesema ni muhimu kwa Ujerumani kupata gesi kutoka Urusi ili kuweza kuendelea kuuimarisha Umoja wa Ulaya. Waziri mkuu wa Slovania ambaye amefanya ziara yake ya kwanza ya nje nchini Ujerumani amesema Ukraine haitanufaika ikiwa nguzo ya Umoja wa Ulaya, Ujerumani itadhoofika. Hata hivyo rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameilaumu Canada iliyofanya matengenezo ya mtambo wa bomba la gesi linaloleta nishati hiyo Ujerumani kutoka Urusi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii