Chelsea Yafikia Makubaliano na Napoli Kumsajili Beki Kalidou Koulibaly

Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza imefikia makubaliano na klabu ya Napoli ya nchini Italia juu ya uhamisho wa Beki wao Kalidou Koulibaly kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 40.

Koulibaly (31) amekuwa kwenye rada za mabingwa hao wa dunia kwa zaidi ya miaka mitano ambapo usajili wake unatajwa kuwa ni mapendekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kocha wa timu hiyo Thomas Tuchel kwa ajili ya kuziba pengo lililoachwa wazi na Antonio Rudiger.

Koulibaly ni beki na nahodha wa timu ya taifa ya Senegal ambayo aliiongoza kuchukua Ubingwa wa Mataifa ya Afrika AFCON mapema mwaka huu.

Aidha klabu ya Chelsea imeendeleza harakati zake za usajili ambapo taarifa zinadai kuwa klabu hiyo ipo katika hatua za mwisho za makubaliano na Manchester City juu ya kukamilisha usajili wa kumrudisha aliyekuwa beki wa klabu hiyo raia wa Uholanzi Nathan Ake kwa ada ya usajili ya paundi milioni 45.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii