Maofisa wa umoja wa Mataifa, juma hili wametangaza kuanzisha uchunguzi kuhusu kujeruhiwa na mauaji ya watoto yaliyofanywa katika nchi za Ukraine, Ethiopia na Msumbiji, wakati huu ripoti zikisema watoto zaidi ya elfu 2 waliuawa tangu mwaka 2021.
Katika ripoti ya kila mwaka kuhusu watoto na mizozo, watoto elfu mbili, mia tano na kumi na tano waliuwa na wengine takriban elfu tano na mia tano kuathirika kutokana na migogoro inayoendelea duniani.
Aidha ripoti hiyo imenakili ukiukaji mwingine wa haki za binadamu ikiwemo utekaji nyara, dhulma za kingono, mashambulio katika shule na hospitali na kunyimwa msaada wakati wa vita.
Katibu mkuu wa umoja wa Matiafa Antonio Guterres amesema katika ripoti ya mwaka ujao, watajumuisha dhulma dhidi ya watoto katika nchi za Ukraine, Ethiopia na Msumbiji.
UN, imebaini ukiukaji wa haki za watoto katika mwaka wa 2021 uliripotiwa katika mataifa ya Yemen, Syria, Afghanistan, Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo, Somalia,Israeli pamoja na Palestina.
Katika ripoti yake ya wiki iliyopiyta mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu Michelle Bachelet, alieleza kuwa zaidi ya raia elfu nne na mia nane walikuwa wameuawa nchini Ukraine, idadi hiyo ikijumuisha watoto 335 idadi hiyo pia ikitajwa kuwa huenda ikaongezeka.