Marekani imetangaza kuongeza kiwango cha riba

Benki kuu ya Marekani ilitangaza Jumatano kuwa itapandisha viwango vya riba kwa kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha takriban miaka 30 ikiwa ni juhudi za kukabiliana na mfumuko wa bei bila ya kuufanya uchumi kudorora.

Benki kuu ilisema itaongeza kiwango chake muhimu cha riba kwa robo tatu ya asilimia, kiasi kikubwa zaidi tangu Novemba mwaka 1994 na kuashiria nyongeza zaidi zijazo.

Kuongezwa kwa kiwango kunakuja wakati mfumuko wa bei ambao unapima bei za bidhaa muhimu kama vile chakula na mafuta zimepanda kwa asilimia 8.6 katika kipindi cha miezi 12 ambayo inaishia Mei kiwango cha juu zaidi katika miaka 40 kilisukumwa na mahitaji ya juu baada ya janga lililoathiri nyumba, magari, usafiri na bidhaa nyingine pamoja na huduma kutokana na matatizo ya mfumo wa usambazaji kwasababu ya masharti ya COVID-19 ya kufungwa kwa shughuli huko China na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Ongezeko la kiwango kwa robo tatu linavuka ongezeko la pointi moja na nusu ambalo mwenyekiti wa benki kuu Jerome Powell awali alipendekeza na kusema huenda lingepitishwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii